Charles WashomaAbout

Kupeleka ujumbe wa matumaini na wa kuhamasisha kuwepo kwa uongozi shirikishi wenye lengo la kujenga jumuiya unganifu na yenye tija za kimaendeleo kwenye nyanja zote za jamii ikiwepo biashara, jamii kwa ujumla na baina ya mataifa mbalimbali. Charles anaamini kuwa mafanikio  yanatokana na mipango yatokanayo na fikra na akili timamu kwaupande wa binadamu. Hatahivyo, yeye anaamini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mwanzishi na Muumbaji wa uhai wetu. Imani yake Charles ni Kuwa na maisha yenye makusudio maalum. Katika mambo anayoyapenda ni pamoja na sanaa, kusafiri ndani ya Afrika na duniani kote, michezo mbalimbali ikiwepo kuruka angani, ameyafanya yote haya wakati yeye akiwapenda na kujivunia watoto wake wanne.

Kwaupande weledi, Charles ni MFANYABIASHARA MWANDAMIZI, MJASIRIAMALI, MWANDISHI WA MAMBO YA JAMII na mwishoni MWONGEAJI MWENYE USHAWISHI MKUBWA

Last from my blog

Subscribe the RSS Feed

Subscribe to Syndicate

Jinsi ya Kuleta Mabadiliko Duniani

9 August 2013 - 12:00am -- charles

(Mabadiliko madogo yanaweza kuleta matokeo makubwa!)

Nilipokuwa mdogo mara nyingi nilikuwa nikihuzunishwa na matatizo yaliyokuwa yanaikabili jamii, na nilijiuliza ni sababu gani zilisababisha watu wateseke kwa umaskini, maradhi na mateso mengine. Kasha niliwaza ni kwa namna gani hali hii inaweza kuboreshwa; nilwaza juu ya ufumbuzi wa kuwasaidia watu maskini au namna ya kuleta aamani ambayo imejaa haipo katika dunia hii, lakini pia nikawaza, “Mimi ni nani wa kudhani kwamba ninaweza kuibadili dunia?”

Umuhimu wa Tunu na Maadili Katika Uongozi!

6 August 2013 - 10:11pm -- charles

Mahusiano yote, mawasiliano na shuhuli katika maisha, iwe ni kwa watu binafsi, makampuni, au yote mawili, ni lazima yasimamiwe na kanuni na viwango. Kanuni hizi na viwango hujengewa kwenye msingi wa tunu ambazo husimamia maamuzi ya wale wanaohusika.

Mameneja na watendaji wana jukumu la msingi la kuweka na kusimamia viwango katika mashirika, na yafuatayo ni baadhi ya maeneo muhimu ambamo wajibu huu ni muhimu:

Faida na Tuzo za Uongozi wenye Mafanikio!

5 August 2013 - 9:35pm -- charles

Kama viongozi wa mashirika, mameneja huchagua shuhuli, mikakati, na mbinu ambazi zitztumiwa na timu katika kutimiza vipaumbele na malengo. Ili kuweza kutimiza hayo wanazo raslimali mbalimbali za kufanikisha hayo, ikiwa ni pamoja na nguvu na hamasa  ya idara au mashirika yao, ubunifu na mawazo, uwezo wa kufanya kazi na rasilimali fedha zilizopo. Kuna faida  na tuzo mbalimbali kwa uongozi bora, na zinajumuisha zifuatazo:

Ninayo maadli saba ambayo kwayo naongoza mwenendo na tabia yangu nazo hizi zifuatazo:

UADILIFU – Mimi ni mkweli na mwaminifu. Maneno na matendo yangu yote yanaendana.

UJASIRI – Nimeutawala uwoga na kutupilia mbali mashaka.

HEKIMA – Ninatofautisha kati ya mabaya na mema, na ninatumia ufahamu huo ipasavyo.

HUDUMA – Nimedhamiria kutoa huduma kwa namna bora zaidi kwa binadamu, nikianzia na familia na jumuia yangu.

KUJIFUNZA – Dhamiria yangu ni kuendelea kujifunze siku zote ili nijikuze kiakili na kiroho.

UJASIRI – Ninayatazama maisha kama safari ndefu ambayo inahitaji isafiriwe kwa ujasiri na hamasa.

UBUNIFU – Ninathamini kwa namna ya pekee uwezo na uhuru wa kuboresha  kile ambacho tayari ninacho. Ninaona njia kuelekea lengo ninalolitamani, na nitajitahidi kuutumia ubunifu ili kufikia lengo husika.