Blog

Subscribe the RSS Feed

Subscribe to Syndicate

Jinsi ya Kuleta Mabadiliko Duniani

9 August 2013 - 12:00am -- charles

(Mabadiliko madogo yanaweza kuleta matokeo makubwa!)

Nilipokuwa mdogo mara nyingi nilikuwa nikihuzunishwa na matatizo yaliyokuwa yanaikabili jamii, na nilijiuliza ni sababu gani zilisababisha watu wateseke kwa umaskini, maradhi na mateso mengine. Kasha niliwaza ni kwa namna gani hali hii inaweza kuboreshwa; nilwaza juu ya ufumbuzi wa kuwasaidia watu maskini au namna ya kuleta aamani ambayo imejaa haipo katika dunia hii, lakini pia nikawaza, “Mimi ni nani wa kudhani kwamba ninaweza kuibadili dunia?”

Umuhimu wa Tunu na Maadili Katika Uongozi!

6 August 2013 - 10:11pm -- charles

Mahusiano yote, mawasiliano na shuhuli katika maisha, iwe ni kwa watu binafsi, makampuni, au yote mawili, ni lazima yasimamiwe na kanuni na viwango. Kanuni hizi na viwango hujengewa kwenye msingi wa tunu ambazo husimamia maamuzi ya wale wanaohusika.

Mameneja na watendaji wana jukumu la msingi la kuweka na kusimamia viwango katika mashirika, na yafuatayo ni baadhi ya maeneo muhimu ambamo wajibu huu ni muhimu:

Faida na Tuzo za Uongozi wenye Mafanikio!

5 August 2013 - 9:35pm -- charles

Kama viongozi wa mashirika, mameneja huchagua shuhuli, mikakati, na mbinu ambazi zitztumiwa na timu katika kutimiza vipaumbele na malengo. Ili kuweza kutimiza hayo wanazo raslimali mbalimbali za kufanikisha hayo, ikiwa ni pamoja na nguvu na hamasa  ya idara au mashirika yao, ubunifu na mawazo, uwezo wa kufanya kazi na rasilimali fedha zilizopo. Kuna faida  na tuzo mbalimbali kwa uongozi bora, na zinajumuisha zifuatazo:

Maswali Kumi Muhimu ya Kutafakari!

5 August 2013 - 11:40am -- charles

Ulimwengu wa sasa uendao kasi na wenye mahitaji mengi mara nyingi huwafanya watu wakose muda wa kukaa chini na kutafakari. Hata hivyo muda hautakuja wenyewe. Kwahiyo tunahitaji kuutafuta muda ili tuweze kutafakari masuala muhimu ya maisha.

Kwahiyo muda unapofika, usiupoteze. Yafuatayo ni maswali mepesi, lakini ya maana ya kuyatafakari: